Jumanne, 30 Septemba 2014

CHAMA CHA WANAWAKE WA AFRIKA WAKABIDHI WASHINE YA KUPIMA SALATANI KWA MAMA SALMA KIKWETE

Chama cha wa Wanawake na wakereketwa wa salatani Afrika wamemkabidhi Mke wa Rais na Mwenyekiti  wa wanawake na maendeleo WAMA Mama Salma Kikwete  mashine ya kupimia salatani kwa wanawake Watanzania kwa thamani ya milion mbili hapo juzi uko Woshington DC.

Wanawake hao wakereketwa wa ugonjwa wa salatani wameamua kutoa mashine katika nchi za Afrika katika kuakikisha kuwasaidia wanawake wa bara la Afrika




Pichani ni Mama Salma kikwete akishukuru baada ya kukabidhiwa mashine ya salatani

Mama Salma kikwete ameshukuru kwa niaba ya watanzania na kusema mashine hiyo itasaidia kupunguza na kuokoa vifo vya wanawake wengi vinavyosababishwa na salatani na kuwasaidia wanawake kufanya uchunguzi wa afya zao mabema ili kubaini kama wanatatizo.

Jumatatu, 29 Septemba 2014

MWANAMKE MBARONI KWA TUHUMA ZA KUTESA MTOTO

Mwanamke mmoja ambae anafahamika kwa jina la mama Rashid mkazi wa kunduchi amejikuta mikononi mwa polic baada ya majirani zake kumvamia nyumbani kwake kwa kosa la kumtesa na kumjeruhi mtoto.

Huku unyama unaofanywa na wanawake umeonekana kuendelea na wakazi wa kunduchi kuchoshwa na vitendo vya mwanamke huyo na kuamua kumshitaki kwa polisi ili kuondoa unyanyasaji na ukatili anaofanyiwa mtoto huyo.

Mtoto Lucy ni binti wa miaka mitano ndiye aliyefanyiwa unyama huo na mama yake wa kambo na alipoulizwa alionekana mwoga wa kuongea chochote huku akimwangalia mama yake wa kambo na kulia.

Majirani wa mwanamke huyo walionekana kukerwa na vitendo vya  unyanyasaji wa mwanamke huyo na kusema kuwaimekuwa ni kawaida yake mara kwa mara kumpiga mtoto huyo na wameamua kumchukulia hatua ili iwe mfano kwa wanawake wengine wanaonyanyasa watoto.

Bibi Boke ni bibi wa mtoto lucy amesikitika kumuona mjukuu wake akiteseka huku akishuhudia alama za fimbo katika mwili wake na kutaka kumsaidia ili kumuwezesha mjukuu wake ambaye ameonekana akikosa haki zake za msingi aweze kuzipata.

Naye mwanamke huyo anashikiriwa na polisi kawe kwa tuhuma za kujeruhi na kumnyima haki za binadam mtoto Lucy.

Alhamisi, 25 Septemba 2014

MAMA SALMA KIKWETE AFUNGUA MKUTANO WA ELIMU KWA VIJANA

   Ni mke wa Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na maendeleo WAMA Mama Salma Kikwete amepewa kipaumbele na kupewa nafasi kubwa ya kufungua mkutano mkubwa ulioandaliwa na serikari ya ujeruman kwa lengo la kujadiri maswala ya Elimu kwa vijana wa wa bara la Afrika ili waweze kufanya maauzi sahihi ya kiafya.
Mama salma kikwete akisalimiana na mke wa katibu mkuu wa mataifa mama yoo Soon  Taek wakati wakiingia kwenye mkutano

Mkutano huo umefanyika uko New York na kuhudhuliwa na viongozi na wageni wengi mashuhuri kutoka nchi tofauti za bara la Afrika ikiwemo waziri wa ushirikiano wa uchumi wa Ujeruman Mh. Gerd Mueller, mke wa Raisi wa malawi Getrude Mutharka, waziri wa Afya wa Botswana na wengine wengi.

Pia amewataka vijana kujitambua na kuelewa elimu ya afya wanayopewa waikubali kwa kuifata ili kulinda afya yao ili kuweza kutimiza malengo waliyojiwekea.

Mama Salma Kikwete alipata fulsa ya kuhutubia Mkutano huo na katika hutuba yake alitoa kipaumbele kwa  wanawake asa vijana katika kupewa elimu ya ziada itakayoweza kuwasaidia kulinda afya yao na kuwataka kuakikisha kukamatwa kwa watu wanaosababisha kuaribu afya ya wanawake kimakusudi.

Jumatano, 24 Septemba 2014

MTOTO MCHANGA ATUPWA TEGETA

Mwanamke mmoja mkazi wa tegeta amemtupa mtoto mchanga chini ya mti na kumtelekeza.


    Ni jambo la kushangaza limewashtusha wakazi wa Tegeta Kibaon Jijini Dar es salaam baada ya baadhi ya wasamaria wema kumuokota mtoto mchanga chini ya mti majira ya asubuhi akiwa mzima.

    Mwenyekiti wa mtaa  huo Maurid Ramadhan amethibitisha kututokea kwa tukio hilo na kusema ameshtushwa na tukio hilo kwani toka awe kiongozi wa mtaa huo ana miaka mitatu sasa na ajawai kushuhudia tukio hilo na kuwaasa wanawake wawe walinzi wa kwanza kwa wenzao na kufanya jitiada za kumkamata mtuhumiwa wa tukio hilo.

     Mmoja wa shuhuda wa tukio hilo amejitambulisha kwa jina la mama Ashimu amesema kuwa alikua akipita eneo la tukio kuelekea kazini kwake ndipo aliposikia sauti ya kichanga kikilia ndipo alipoifatilia sauti na kumkuta mtoto mchanga akiwa amewekwa chini ya mti akiwa amifungwa kaka moja.

   Matukio ya kutupa watoto yamekua ni janga kutokana na kuongezeka siku adi siku. Ni jambo linalosikitisha kuona mwanamke anafumilia shida zote na kujaariwa adi kujifungua salama na kufikia hatua ya kumtupa mtoto huku tunaona bado kuna wanawake wengi wanatafuta watoto. Unafikiri nini chanzo cha wanawake kutupa watoto na nini kifanyike kumaliza tatizo hili?