Mwanamke mmoja ambae anafahamika kwa jina la mama Rashid mkazi wa kunduchi amejikuta mikononi mwa polic baada ya majirani zake kumvamia nyumbani kwake kwa kosa la kumtesa na kumjeruhi mtoto.
Huku unyama unaofanywa na wanawake umeonekana kuendelea na wakazi wa kunduchi kuchoshwa na vitendo vya mwanamke huyo na kuamua kumshitaki kwa polisi ili kuondoa unyanyasaji na ukatili anaofanyiwa mtoto huyo.
Mtoto Lucy ni binti wa miaka mitano ndiye aliyefanyiwa unyama huo na mama yake wa kambo na alipoulizwa alionekana mwoga wa kuongea chochote huku akimwangalia mama yake wa kambo na kulia.
Majirani wa mwanamke huyo walionekana kukerwa na vitendo vya unyanyasaji wa mwanamke huyo na kusema kuwaimekuwa ni kawaida yake mara kwa mara kumpiga mtoto huyo na wameamua kumchukulia hatua ili iwe mfano kwa wanawake wengine wanaonyanyasa watoto.
Bibi Boke ni bibi wa mtoto lucy amesikitika kumuona mjukuu wake akiteseka huku akishuhudia alama za fimbo katika mwili wake na kutaka kumsaidia ili kumuwezesha mjukuu wake ambaye ameonekana akikosa haki zake za msingi aweze kuzipata.
Naye mwanamke huyo anashikiriwa na polisi kawe kwa tuhuma za kujeruhi na kumnyima haki za binadam mtoto Lucy.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni