Jumatano, 24 Septemba 2014

MTOTO MCHANGA ATUPWA TEGETA

Mwanamke mmoja mkazi wa tegeta amemtupa mtoto mchanga chini ya mti na kumtelekeza.


    Ni jambo la kushangaza limewashtusha wakazi wa Tegeta Kibaon Jijini Dar es salaam baada ya baadhi ya wasamaria wema kumuokota mtoto mchanga chini ya mti majira ya asubuhi akiwa mzima.

    Mwenyekiti wa mtaa  huo Maurid Ramadhan amethibitisha kututokea kwa tukio hilo na kusema ameshtushwa na tukio hilo kwani toka awe kiongozi wa mtaa huo ana miaka mitatu sasa na ajawai kushuhudia tukio hilo na kuwaasa wanawake wawe walinzi wa kwanza kwa wenzao na kufanya jitiada za kumkamata mtuhumiwa wa tukio hilo.

     Mmoja wa shuhuda wa tukio hilo amejitambulisha kwa jina la mama Ashimu amesema kuwa alikua akipita eneo la tukio kuelekea kazini kwake ndipo aliposikia sauti ya kichanga kikilia ndipo alipoifatilia sauti na kumkuta mtoto mchanga akiwa amewekwa chini ya mti akiwa amifungwa kaka moja.

   Matukio ya kutupa watoto yamekua ni janga kutokana na kuongezeka siku adi siku. Ni jambo linalosikitisha kuona mwanamke anafumilia shida zote na kujaariwa adi kujifungua salama na kufikia hatua ya kumtupa mtoto huku tunaona bado kuna wanawake wengi wanatafuta watoto. Unafikiri nini chanzo cha wanawake kutupa watoto na nini kifanyike kumaliza tatizo hili?


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni