Ni mke wa Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na maendeleo WAMA Mama Salma Kikwete amepewa kipaumbele na kupewa nafasi kubwa ya kufungua mkutano mkubwa ulioandaliwa na serikari ya ujeruman kwa lengo la kujadiri maswala ya Elimu kwa vijana wa wa bara la Afrika ili waweze kufanya maauzi sahihi ya kiafya.
![]() |
| Mama salma kikwete akisalimiana na mke wa katibu mkuu wa mataifa mama yoo Soon Taek wakati wakiingia kwenye mkutano |
Mkutano huo umefanyika uko New York na kuhudhuliwa na viongozi na wageni wengi mashuhuri kutoka nchi tofauti za bara la Afrika ikiwemo waziri wa ushirikiano wa uchumi wa Ujeruman Mh. Gerd Mueller, mke wa Raisi wa malawi Getrude Mutharka, waziri wa Afya wa Botswana na wengine wengi.
Pia amewataka vijana kujitambua na kuelewa elimu ya afya wanayopewa waikubali kwa kuifata ili kulinda afya yao ili kuweza kutimiza malengo waliyojiwekea.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni