Jumatano, 29 Oktoba 2014

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MAONYESHO YA MWEZI YA WANAWAKE WAJASILIAMALI (MOWE)

Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. Mohammed Gharib Bilal,jana amekua mgeni rasmi katika maonyesho ya mwezi wa wanawake wajasiliamali (WOMA) uliofanyika jijini Dar es salaam ukiwa na lengo la kuwatambua wanawake wanaojishughurisha katika biashara mbalimbali ili kuwahamasisha wanawake wengine ambao nao wanatamani kuwa wajasiliamali na wale wasijishughulisha kuasishika.

 9

Katika ufunguzi huo Dkt Bilali ametembelea mabanda ya wanawake hao na kujionea biashara zinazofanywa na wajasiriamali huku akionekana kurizishwa na kazi zao pia aliwasapoti kwa kununua baadhi za bidhaa walizoziuza na kuataka kuendeleza bidii katika biashara zao ili na wao wasiwe tegemezi.

 4

 Pia maonyesho hayo yameshuhudiwa na viongozi  mbalimbali ambao nao walijaribu kuzidi kuwahamasisha wanawake hao wajasiliamali kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kupata maendeleo yao na taifa kwa ujumla na si kusubilia maonyesho kama kutengeneza bidhaa zao.
 
11
Makamu wa Rais Dkt Bilali katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa vikundi mbalimbali na wageni waalikwa katika maonyesho hayo.
 

WANAWAKE WAMEHAMASISHWA KUTUMIA FULSA ILIYOPO KATIKA SEKTA YA BAHARI

Wanawake wameaswa kutumia fursa iliyopo katika sekta ya bahari kwa kupata elimu na mafunzo ya sekta hiyo ambayo ni msingi wao katika kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia ukuaji sayansi na teknolojia inayoongezeka kwa kasi duniani.
 
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Usalama wa Mazingira Majini Tumpe Mwaijande kutoka Wizara ya Uchukuzi kwaniaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Shaaban Mwinjaka wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa Umoja wanawake walio katika Sekta ya masuala ya Bahari Mashariki na Kusini mwa Afrika (WOMESA) ulifanyika jana  Dar es salaam.
 

unnamed2
Mwenyekiti wa WOMASA kutoka Mauritius Bi. Meenaksi Bhirugnath Bhookun akitoa mada wakati wa ufunguzi wa mkutano huo
Akisoma hotuba kwa niaba ya Katibu Mkuu huyo, Mwaijande amewataka wajumbe wa mkutano huo (WOMESA), wawe tayari kujadili masuala yanayojenga na kukuza ushiriki wa wanawake katika sekta ya bahari katika nchi zao.
 
Katika mkutano huo wa siku nne ambao umeanza leo oktoba 28 na unatarajiwa kumalizika Oktoba 31 mwaka huu, mada mbalimbali zitajadiliwa ikiwemo mpango mkakati wa WOMESA kuhusu ushiriki wa wanawake katika masuala ya sekta ya bahari katika nchi wanachama. 
 
Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi kutoka Shirika la Kimataifa linaloshughulikia Mambo ya Bahari (IMO) Pamela Tansey amesema kuwa WOMESA imekuwa msatari wa mbele katika kumwendeleza mwanamke kwenye sekta ya bahari.
 
unnamed4
Picha ya pamoja ya wajumbe wa mkutano wa mwaka wa WOMASA mara baada ya ufunguzi wa mkutano huo.
Pamela amesisitiza kuwa wajumbe wa mkutano huo ni vema waelewe na kusimamia dira ya WOMESA ambayo lengo lake ni kuwawezesha wanawake kupata ajira katika sekta ya masuala ya bahari kwa njia ya kupta elimu na mafunzo katika kuendeleza taaluma yao juu ya masuala ya bahari.
 
Mkutano huo wa WOMESA unajumuisha wajumbe 52 kutoka nchi mbalimbali wanachama zikiwamo Ethiopia, Namibia, Komoro, Visiwa vya Shelisheli, Zambia, Mauritius na Kenya. 
 
Nchi nyingine ni Angola, Sudani, Lesotho, Uganda, Somalia, Eritrea, Botswana, Rwanda, Madagaska, Afrika Kusini, Msumbiji, Burundi, Malawi, Djibout, Zimbabwe na wenyeji Tanzania.
 
Mkatano huo wa siku nne unafanyika nchini chini ya ufadhili wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Taasisi ya Masuala ya Bahari Tanzania (DMI),   shirika la mfuko wa hifadhi ya jamii (NSSF) kwa kushirikiana na  Shirika la Kimataifa linaloshughulikia Mambo ya Bahari (IMO) na Shirika la Kimataifa la Maendeleo (UNDP).
 

Jumanne, 28 Oktoba 2014

MWENYEKITI MWENZA WA TAASISI YA BILL AND MELINDA GATES ASEMA WAWEZESHENI WANAWAKE KUISAIDIA AFRIKA

Licha ya uwepo wa fikra tofauti juu ya maendeleo kwa wanawake mfadhili Melinda Gates, anaamini ukitaka kuisaidia Afrika kwanza anza na wanawake kwa kuwa ni ufunguo katika kukuza uchumi na maendeleo Afrika

Burundi Landwirtschaft Kilimo cha wanawake nchini Burundi

Bi Melinda akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mjini Paris hivi karibuni , kuhusu mradi wa kuchangisha fedha kwa ajili ya wanawake na wasichana alisema kuwawezesha wanawake ni miongoni mwa malengo yenye kipaumbele chenye nguvu katika taasisi ya Bill na Melinda Gates katika mkakati wa kuwasaidia watu katika nchi zinazoendelea kuwa huru katika nyanja ya afya, uzazi wa mpango na hali ngumu ya maamuzi kuhusu uchumi.

Hii ni kutokana na kuwa na ushahidi unaoonyesha wanawake barani Afrika , Asia na Amerika kusini wanauwezo mkubwa wa kuweka akiba ya fedha na kuirudisha katika matumizi ya familia kuliko wanaume wanavyofanya. Ambapo kuweka akiba huko kuna msaada kwa familia ya mwanamke na jamii kwa ujumla hali ambayo inashawishi kuwasaidia wanawake na wasichana katika maendeleo.

Kama kuna haja ya kukuza uchumi barani Afrika ni lazima uanze na wanawake licha ya kuwa mengi yanasemwa kuhusu mahitaji ya kuwawezesha wanawake ikiwemo ya kuzingatia katika kupunguza idadi ya uzazi na kuongeza jitihada za afya ya uzazi ambayo ni mkakati wa pili kati ya nane wa maendeleo ya milenia uliowekwa mwaka 2000 na jitihada kubwa zimefanywa kulisogeza hilo mbele.

Forbes Liste Die mächtigsten Frauen der Welt Melinda Gates Mwenyekiti mwenza wa taasisi ya Bill and Melinda Gates

Melinda amefafanua kuwa vifo vinavyotokana na uzazi vimepungua mara tatu kwa miaka 30 iliyopita na vifo vya watoto wachanga vimepungua kwa nusu ya ilivyokuwa kabla ya mpango huu. Makundi ya misaada yanafanya kazi kwa mpango mpya wa Milenia wenye lengo la kukuza usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake ambako kutasaidia kupunguza umasikini na njaa.

Kwa mujibu wa ripoti ya kilimo na chakula ya Umoja wa mataifa ya mwaka 2010 -2011, kama wanawake watashirikishwa katika kilimo kwa nchi zinazoendelea kutaongeza mazao na hatimae kutasaidia kupunguza idadi ya watu wanaokosa chakula kwa asilimia 12 mpaka 17.

MWANAMKE APIGWA NA MUMEWE HADI KUFA HUKO MKOANI MOROGORO

Bado ukatiri unaofanywa na wanaume kwa wake zao unaenderea kuripotiwa huku ikiwa jamii ikitahayari kuona Katibu mkuu wa CCM Mkoa wa morogoro Bi. Rozina kopa ameuwawa baada ya kupigwa na mumewe huku chanzo cha kupigwa kwake adi kufa bado hakijafahamika.

Marehemu bi. Rozina kabla ya kifo chake inasemekana baada ya kukorofishana na mumewe nyumbani aliamua kuondoka ili akwepe ugomvi kuenderea ndipo mtuhumiwa wa mauaji hayo Hamis Tata ambaye ni mume wa marehemu alimsaka tena mkewe na ndipo alipomkuta kwenye bar ya mafiga bar na kuanza kumpiga.

Mashuhuda wa tukio hilo akiwemo bwana mmoja aliyefahamika kwa jina la Rajabu alisema yeye ameshuhudia tukio hilo na alijaribu kumzuia mtuhumiwa kumpiga huku marehemu akionekana anavuja sana damu hasa sehemu za usoni na ndipo mtuhumiwa alimuacha kumpiga mkewe.

 Kwa upande wa  ndugu wa marehemu wamesema ndugu yao baada ya kupigwa sana pale bar waliporudi nyumbani mtuhumiwa aliendelea kumpiga mkewe na kumuingilia kimapenzi bila idhini yake
kabla mauti haijamkuta walimkimbiza hospitali ya mkoa uku akiwa akilalamika kifua kumuuma sana .

Naye kamanda wa polisi mkoani morogoro amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na adi sasa wanamshikiria bw. Hamis Tata kwa tuhuma za mauaji.

Hili ni moja ya tukio baya ambalo bado linazidi kuongeza idadi ya vifo vya kinyama vinavyofanywa na wanaume kwa wake zao na hatimaye mwili wa Bi Rozina Tata umezikwa katika makaburi ya kora huko mkoani Morogoro.

SCANDAVIA YAONGOZA UWIANO WA KIJINSIA

Katika ripoti mpya ya mwaka iliyoitoa Jukwaa la kiuchumi duniani inaonyesha nchi za Scandavia zinaongoza kwa uwiano wa kijinsia kwa kuangaza fulsa kwa wanawake katika nchi 142 huku nchi za Afrika zikiongozwa na Rwanda.

Miongoni mwa mambo yaliyozingatiwa katika ripoti hiyo, Kwanza, wanawake wanafanyakazi na kulipwa malipo sawa kwa kazi iliyosawa na nafasi ya kupata elimu.

Maeneo mengine yaliyozingatiwa ni kweli wanawake wanaruhusiwa kushiriki katika masuala ya kisiasa haswa katika ngazi za juu, kuweza kushika nafasi za ubunge na hata madaraka ya juu zaidi Nchi zilizotajwa katika ripoti hiyo kuongoza ni Iceland ikifuatiwa na Norway, Finland, Sweden, Denmark.

Phillipines nchi iliyo katika bara Asia imeshika nafasi ya tisa. Rwanda imeibuka kidedea kwa kuweza kuingia katika 10 bora ya nchi hizo 142, ambazo zilifanyiwa utafiti na pia kuwa nchi ya kwanza ya Afrika na zinazoendelea kuweza kushika nafasi ya kwanza katika ripoti hiyo.

Mafanikio ya Rwanda yanatokana na uwezo wa kupata huduma za afya na elimu, lakini pia, yanaangazia idadi kubwa ya wanawake wanaoshika nafasi za uwaziri.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo mafanikio ya wanawake yanazidi kuonekana, kwani sasa kuna asilimia 26 zaidi ya wanawake wabunge duniani kote na asilimia 50 zaidi ya wanawake mawaziri kushinda ilivyokuwa miaka 10 iliyopita.

Utafiti huo uliofanywa umeonesha pia kuwa pengo kubwa katika usawa wa kijinsia lipo katika nchi za Chad, Pakistan na Yemen, ambako hakuna mabadiliko na mwaka uliopita.

Jumatatu, 27 Oktoba 2014

MAHAFALI YA PILI YA SHULE YA WAMA NAKAYAMA YAFANYIKA HUKU UBALOZI WA JAPANI WAISAIDIA SHULE HIYO SH. MILIONI 800

 Ubalozi wa japan kupitia wizara ya Mambo ya Nje umetoa msaada wa kiasi cha fedha cha sh. Milioni 800 ambazo ni sawa na dola za Kimarekani 500,000 kwa ajiri ya kusaidia Shule ya Sekondari ya wasichana wanaoishi katika maisha magumu na hatarishi ya WAMA Nakayama, iliyopo wilayani Rufiji mkoani pwani.

Hayo yalisemwa jana na Kaimu Balozi wa japan nchini Kazuyoshi Matsu Naga wakati wa sherehe za mahafari ya pili ya shule hiyo yaliyofanyika jana na kuhudhuliwa na Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha Rose Migiro ambaye alikua mgeni rasmi baadhi ya viongozi wengine wakiwemo baadhi ya wake wa wageni wengine mbalimbali.
 
IMG_8872
Waziri wa Katiba naSheria Dkt Asha Rose Migiro (katikati)  Akiwa na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendereo WAMA Mama  Salma Kikwete  pamoja na Kaimu balozi wa Japani.
Kwa upande wake, Dkt. Migiro, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo, aliwataka  wadau mbalimbali  kuendelea kumsaidia Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Salma  Kikwete  katika kusaidia wanafunzi hao ili kupanua fursa za watoto wa kike kielimu 
Naye Mke wa Rais Mama Kikwete, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) aliwataka  wanafunzi hao  kutumia nafasi ya kusoma  bidii  ili waweze kufaulu hatimaye  kushika nafasi mbalimbali  za  uongozi kama Dkt.

Akizungumzia kuhusu matarajio ya WAMA kutokana shule hiyo, alisema kutoa wataalamu wa nyanja zote , ikiwemo fani ya sayansi . Hivyo  aliwataka kuongeza bidii katika masomo ya sayansi. Alisema WAMA itaendelea kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu hadi watakapofikia hatua  ya mwisho.

3
Wahitimu wa elimu ya sekondari kidato cha nne katika shure hiyo ya WAMA  wakati wa sherehe yao ya kumaliza
 Waziri  wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu,  Tawala  za Mikoa na Serikali za Mitaa Tamisemi (TAMISEMI) Hawa Ghasia aliwapongeza walimu wa shule hiyo kwa bidii zao ambao zimeifanya shule hiyo  kuongeza katika wilaya hiyo.

MSICHANA ALIYETOROKA ASIMULIA YA BOKO HARAM



Ni mmoja ya wasichana waliotekwa na Boko Hatam na kutoroka na kusimulia yaliyokua yakitokea wakati akizungumza katika mahojiano maalum na idhaa ya Kihausa ya BBC, Msichana huyu anakumbuka jinsi alivyokuwa nyuma ya Lori wakati wapiganaji wa Boko Haramu walipomteka yeye na wasichana wengine.

'' nilikuwa nataka kurukia nje wakati msichana mwenzangu aliponikamata kwa nyuma na kusema watakupiga risasi kama utafanya hivyo. Nikasema, nini utofauti wataniua mimi hapa na kuacha maiti yangu ikabaki nilikuwa nalia na kuomba mpaka tulipoifikia kambini" Anasimulia msichana mmoja alitoroka mikononi mwa Boko Haram.

Ni miezi sita sasa baada ya wanamgambo wa kiislam wa kundi la Boko Haram kuwateka wanafunzi wasichana Zaidi ya 200 kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Tukio hili linakuja wakati serikali ya Nigeria ikiwa katika makubaliano ya kusimamisha mapigano dhidi ya Boko Haram hatua itakayo saidia kuwaachilia huru wasichana waliotekwa na kundi hilo .

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binaadam la Human Rights Watch limesema wanawake wanaoshikiliwa na kundi la Boko Haramu wamekuwa wakinyanyaswa, kubakwa na hata kulazimishwa kuolewa.

Katika ripoti mpya ya shirika hilo inasema Wanamgambo hao wa Kiislam wamewateka wanawake Zaidi ya 500 na wasichana tangu mwaka 2009.

Serikali ya Nigeria hivi karibuni imetangaza makubaliano ya kusimamisha mapigano dhidi ya Boko Haram ambayo hatua itakayawafanya wanamgambo ho kuachilia huru wasichana wa hao waliotekwa huko Chibok.

Lakini Boko Haram wenyewe hawajawahi kuthibitisha makubaliano yoyote ya kusitisha mapigano na hakuna dalili zozote za kuachiwa kwa wasichana haohivi karibuni.

Lakini kwa wale waliobahatika kutoroka, matatizo ya kisaikolojia bado yanawasumbua..

Ijumaa, 24 Oktoba 2014

NI KWELI MATESO AMEUMBIWA BINADAMU ILA HUYU BINTI HAYA NI MATESO YAKE

Binti wa miaka 20 aliyetambulika Riziki Haji mkazi wa Kijiji cha Kondo mkoa wa Pwani, wilayani Bagamoyo, yupo kwenye mateso makali kutokana na ugonjwa wa kifafa unaomsumbua kwa muda mrefu!
Riziki ambaye aliugua ugonjwa wa kifafa akiwa na umri wa miezi nane, amekuwa akiishi katika mazingira magumu kiasi cha kufungiwa ndani usiku na mchana.
 

 


 

 Aidha, imeelezwa kipindi cha mvua na baridi binti huyo huwa katika hali mbaya zaidi kutokana na makuti yaliyotumika kutengenezewa kibanda hayahimili hali hizo.
Akisimulia tukio hilo, jirani wa karibu na sehemu anayoishi Riziki kwa sharti na kutoandika jina lake, alisema Riziki amekuwa katika maisha mabaya kwa muda mrefu huku wazazi wake baba na mama wakitupiana mpira mtu sahihi wa kuishi nae.
“Baba wa Riziki yupo Zanzibar na anafahamu vizuri sana hali ya mtoto wake lakini wala hakuna msaada anaotuma….kuna muda mama yake aliamua kumpelekea lakini siku chache baadae alimrejesha kwa mama yake! Lakini pamoja na kumrudisha mama pia alimkataa na wasamaria wema wakamchukua na kuishi nae,” anasema jirani huyo.
Jirani huyo alibainisha kuwa akiwa anaendelea na maisha kwa msamaria huyo huku akionekana mwenye afya njema, alikuja bibi yake (mama mzazi wa mama wa Riziki) na kumchukuwa na kwenda kuishi nae Bagamoyo ambapo siku chache baadae alimrudisha kwa mama yake mzazi akidai ameshindwa kuishi nae.
Naye Juma Amani Pazi, mwenyekiti wa eneo hilo, mbali na kukiri mazingira ya Riziki kuwa mabaya, pia alisema alikuwa hana taarifa kama katika eneo lake kuna mlemavu anayeishi katika mazingira hatari kama hayo.

UNYAMA UNAOFANYWA NA WADADA WAKAZI ZA NDANI KWA WATOTO WAZIDI KUA TISHIO

Hausigeli aliyejulikana kwa jina moja la Ester (14) yupo matatani kwa madai ya kumuua mtoto Arafat Allan (3) kwa kumnyonga shingo na kumpiga na kitu kizito kichwani kisha kuutumbukiza mwili wake kwenye dimbwi la maji machafu,
Pichani ni mwili wa mtoto Alafat anayedaiwa kunyongwa kisha kutupwa kwenye dimbwi la maji
 Akizungumza kwa uchungu, mama mzazi wa mtoto huyo, Zakia Peter ambaye amelazwa katika Zahanati ya Kellen kutokana na mshtuko wa kifo cha mwanaye, alisema siku ya tukio, hausigeli huyo aliyekuwa na siku mbili tangu aanze kazi aling’ang’ania kutumwa sokoni saa mbili asubuhi ambapo alimkubalia na kumuagiza mboga.


Mama wa marehemu aliendelea kusema kuwa zoezi la kumsaka msichana huyo na mtoto wake liliendelea mpaka Jumanne iliyopita ambapo habari zilisambaa kwamba kuna maiti ya mtoto wa kiume imekutwa ikielea kwenye dimbwi la maji machafu linalotumika kumwagilia bustani za mboga maeneo hayo.

Mama wa mtoto akiwa ospitali baada ya kuzimia



Hili ni moja ya tukio ambayo yamekua yakilipotiwa yanayofanywa na wadada wakazi hii iwakumbushe wanawake wengine kuwa na hisporia nzuri ya wasichana wanowachukua ili kuepuka matatizo kama haya.

MBUNGE WA JIMBO LA TEMEKE ABBAS MTEMVU AFUNGUA VIKOBA

Mbunge wa Jimbo la Temeke Mh.Abbas Mtemvu amefungua vikoba kwa lengo la kuwanufaisha wananchi asa wa Temeke ili kuakikisha vikoba viwasaidie kupata fedha kwaajiri ya kufanikisha maitaji yao pindi wanapoitaji kukopa.



Mbunge  mh Abbas Mtemvu akikabidhiwa T shirt wakati akifungua mfuko huo wa vikoba


Ufunguzi huo umefanyika katika Viwanja vya TCC Clud Jijini Dar es salaam Mbunge huyo  amewataka wananchi kutumia mfuko huo kwa kuweka fedha ambazo zitawasaidia pindi watakapokuwa wanamaitaji makubwa ya fedha hizo na kuwasisitizia kuhushimu mfuko huo kwakua utakua ni mali yao.

Pia Mh. Mtemvu amewataka wanawake kuutumia mfuko huo katika kuakikisha wanatumia fulsa hiyo katika kuhakikisha wanakamilisha mipango yao ya kifamilia na maendeleo.

Baadhi ya wanachama wakishuhudia uzinduzi wa vikoba hivyo



Alhamisi, 23 Oktoba 2014

WANAWAKE KUSHAURIWA KUTUMIA DAWA ZA UZAZI WA MPANGO KUPUNGUZA WATOTO WA MITAANI

Katika kuakikisha kupunguza idadi ya watoto wa mitaani wanawake wametakiwa kuwa wa kwanza kuwashauri waume zao katika kutumia dawa za uzazi wa mpango ili kupanga uzazi wao na kuzaa watoto ambao wanamudu kuwalea bila kuhitaji msaada wa serikari katika kulea watoto wao na hii itasaidia kupunguza idadi kubwa ya watoto wa mitaani.

Waziri wa Afya na ustawi wa jamii Dkt. Seif Rashid  amesema matumizi ya dawa hayo yapo salama kwa mtumiaji na hivyo kuwataka wazazi wakubaliane katika kufanya maamuzi ya kutumia dawa hizo ili kujenga familia iliyo bora isiyokua na ugumu wa kuendelea hii itasaidia kupunguza idadi ya watoto wa mitaani Alisema hayo wakati akikagua utekelezaji wa mipango yake katika mkoa wa Shinyanga.


Aliendelea kusema kuwa wanawake wanatakiwa kufika katika vituo vya afya vilivyo karibu nao ili kupatiwa vipimo na ushauri kabla ya kutumia dawa izo ili kuakikisha afya zao zinakua nzuri na pindi wanapokua tayari kwa kupata mtoto mwingine waweze kwa wakati.

Hata hivyo watoto wa mitaani wamekuwa wengi ambao wameonekana wakiomba omba mitaani huku wengi wao wakikosa haki zao za msingi kama elimu huku wengine wakijiunga katika makundi hatarishi kama ulevi japo zipo sababu mbalimbali zinazosababisha lakini tatizo la wazazi kutokua na uzazi wa mpango unawafanya kushindwa kumudu kutekeleza mzjukumu kwa watoto wao.

Jumatano, 22 Oktoba 2014

WANAWAKE WAJANE WAANDAMANA KUDAI HAKI ZAO

Kikundi cha wanawake ambao ni wajane wameamua kuandamana hadi katika ofisi ya mkuu wa mkoa  wakimshinikiza kupata haki ya mali zao walizoachiwa na waume zao ambazo wamekua wakizifatilia kwa muda mrefu bila mafanikio  huko mkoani Morogoro.

Maandamano hayo ya amani yamefanywa na wanawake hao ili kumtaka Mkuu wa Mkoa atoe kauli yake kwa mamlaka usika ili kuakikisha wanapatiwa kwa haraka mali zao kutokana na kusubiria kwa muda mrefu bila mafanikio na kila wanapojaribu kufatilia upata usumbufu na kubadirishiwa tarehe za kufatilia.

"Tumeamua kuungana na kufanya maandamano haya ya amani ili kupaza sauti zetu kwa Muheshimiwa Mkuu wa Mkoa ili aweze kutusaidia kupata haki yetu tulioachiwa na waume zetu ikiwa walifanya kazi na hili tunalolitafuta sisi ni jasho waliloliangaikia kwa muda mrefu walipokua hai", alisema mmoja wa wanawake hao walioandamana.

Nae Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Bw.Joel Bendela amewahaidi wanawake hao wajane kwa kuwataka wawe na moyo wa uvumilivu huku yeye akivaa malalamiko yao kwa lengo la kuyatatua kwa haraka kama wanavyoitaji na kuwaambia kuwa ni haki yao na atafanya uchunguzi kwa yeyote mwenye lengo la kuwazurumu haki yao itakapo bainika atawaajibisha

Jumanne, 21 Oktoba 2014

JOYCE KIRIA WA WANAWAKE LIVE AMSAKA MUMEWE


Mtangazaji wa kipindi cha wanawake live kinachorushwa na EATV ameamua kuandama pamoja na wanawake wenzake akiwa amewabeba watoto wake wawili waitwao Lincorn na Lingatone  na kuzungumza na waandishi wa habari  nje ya jengo la idara ya Habari Maelezo  iliopo katika mtaa wa samora jijini Dar es salaam uku akipaza sauti kuomba Rais Jakaya Kikwete na Watanzania kwa ujumla ili kusaidia kujua alipo mumewe Bw. Henry Kileo  ambaye inadaiwa kuwa ameshikiriwa na polisi




Akiwa ameonekana mwenye uzuni ameamua kupaza sauti ili kuakikisha mumewe anapatikana hii ikiwa ni ishara ya kuonyesha kutaka msaada wa mumewe katika kuhakikisha wanawalea watoto wao kwa pamoja na kuamua kuwabeba watoto wake hao

Pia katika maandamano hayo ameamua kubeba mabango yenye maneno yanayosema "mume wangu upo wapi" na mabango mengine yalisomeka "Baba yangu uko wapi?".

MIGOGORO YA UMILIKAJI ARDHI KWA WANAWAKE BADO UNAENDELEA KUTOKEA

Bado jamii aijaelewa na kutambua kuwa mwanamke nae ana haki ya kumiliki ardhi na kusababisha mgogoro mkubwa kuendelea huku baadhi ya wanawake wameanza kuelewa haki zao na kuanza kupigania.

 Serikali imeweka dhamira ya dhati katika kuhakikisha mwanamke anatakiwa kupata haki sawa na mwanaume pia na kuweka mkakati wa kuweka sheria ambayo inamruhusu mwanamke kumiliki ardhi.

Hata hivyo chama cha wanasheria wanaweke nchini Tanzania (TAWLA) kimeamua kufanya utafiti kuhusu migogoro ya ardhi inayowakabiri wanawake na kurudi na majibu ambayo utafiti huo uliosisha  mikoa ya Dar es salaam na Tanga.


Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake wanasheria Tanzania (TAWLA) Aisha Bade (kulia) akitoa ufafanuzi 

Vile vile Mwenyekiti wa  Chama cha Wanawake wanasheria Tanzania Aisha Bade amesema lengo la kufanya tafiti hiyo ni kufahamu wanmeathirika kiasi gani ili kuhakisha kuwa wanawake nao wanaweza kumiliki ardhi kwa mujibu wa sheria ambayo itapitishwa.

Pia wamewataka wanawake kuwa na misimamo yao ambayo itawasaidia kutopoteza haki zao za msingi na kutoficha matatizo ambayo wanakumbana nao na kuweka adharani ili kufanya kupata misaada ya kisheria.

Jumatatu, 20 Oktoba 2014

MKUU WA WILAYA YA SAME AMEKIRI ONGEZEKO LA MIMBA ZA UTOTONI NA UKEKETAJI KUSHIKA KASI KATIKA WILAYA YAKE

MKUU wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro, Herman Kapufi, amekiri kuwa Halmashauri ya Wilaya hiyo imezidiwa nguvu na wazazi ambao wanashirikiana na watuhumiwa wanaowapa mimba Wanafunzi ambao hawajamaliza masomo katika shule za Msingi na Sekondari Wilayani humo.

Kapufi ameyasema hayo wakati akiongea katika mazungumzo maalumu na waandishi wa habari, ambapo alidai jambo linaloisumbua Wilaya hiyo ni pamoja na watoto kukeketwa katika umri mdogo wakati Halmashauri ya Wilaya ikiwa inafanya juhudi za kuwakamata wanaoshiriki vitendo hivyo.

Hata hivyo alisema, katika kipindi cha mwaka jana takribani wanawake 37 wamekamatwa na Jeshi la Polisi katika eneo la Kavambughu wilayani humo wakiwa wanawakeketa watoto wachanga ambapo wamefikishwa mahakamani kujibu tuhuma dhidi yao (kesi bado inaendelea).

“Sheria za Nchi zinasema Msichana asiolewe akiwa na umri chini ya miaka kumi na nane awe anasoma au hasomi na kimsingi na wale wanaowakeketa wakiwa wadogo kabla hawajakomaa ili tusigundue bado tunaendelea kufanya uchunguzi ili kuwafikisha katika vyombo vya dola” alisema Kapufi

Takwimu zinaonyesha Wilaya ya Same imekuwa kinara wa kukeketa watoto wachanga na hivyo tatizo hilo kuwa sugu katika Wilaya hiyo.

Afisa Utawala wa Shirika lisilo la kiserikali linalojihusisha na maendeleo ya mwanawake Afya na Haki za Binadamu (LUDEF), Janeth Malibwi, alisema bado mila za ukeketaji katika Wilaya hiyo zinaendelea na kwamba kwa sasa wanakeketa watoto wachanga (pindi wanapozaliwa), jambo ambalo ni hatari kwa Afya zao



MATUKIO YA UTEKAJI WA WATOTO NA MAUAJI YA WANAWAKE YANAENDELEA KUCHUKUA SURA MPYA

Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la mama Debora ameuwawa kwa kukatwa  mapanga yeye pamoja na watoto wake wawili na watu wasiojulikana huko Mkoani Bukoba na kufanya matukio ya utekaji wa watoto na kuuwawa kwa wanawake kushika kasi hapa nchini.

Kamanda wa polisi mkoani Bukoba amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kutoa tamko kwa wananchi kwa ambao wanajiusisha na matukio kama haya watakapo kamatwa hawatakuwa na msamaha na kufuata sheria ili kuakikisha matukio haya hayawi endelevu.

Ni siku chache zimepita toka mwanamke mmoja kunyweshwa madawa ya kulevya na kuibiwa mtoto bado kuna matukio mengi yanaendelea kutokea ya kuibiwa kwa watoto ambao wamekuwa wakiuwawa na watu wasiojulikana na wengi wao kuibiwa.

Hata hivyo kamanda wa polisi mkoa wa Dar es salaamamewatoa hofu wananchi kwa amekanusha maneno ya watu yanayovuma ya kuwa wapo watu ambao wanatumia gari aina ya Noah na kuteka watoto na kuwataka wazazi kuwa walinzi wa watoto wao huku uchunguzi ukiendelea kufanyika kuhusu matukio hayo ambayo yanaendelea na kuwataka wazazi kuwaacha wototo waende shule.

DSC_0212

MJADALA WA SAUTI KUHUSU NDOA ZA UTOTONI

Tuungane kusikiliza mjadala huu wa wanawake kutoka CHAWAWATA kuhusu ndoa za utotoni.

Ndoa za utotoni

Alhamisi, 16 Oktoba 2014

SIKU YA KIMATAIFA YA WANAWAKE VIJIJINI YAFANYIKA JANA KWA LENGO LA KUWASAIDIA HASA KWENYE SEKTA YA KILIMO

Ikiwa jana ni siku ya kimataifa ya wanawake wa vijijini, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amesema kundi hilo linaweza kuchagiza maendeleo ya dunia iwapo sauti na mahitaji yao yatazingatiwa. Maadhimisho hayo yamefanyika jana oktoba 15 yakiwa na lengo la  Kuwaunga mkono wakulima wanawake kwa lengo kuwasaidia kushinda balaa la njaa.

 

 

Na kwa hapa nchini Tanzania  Mkurugenzi wa Oxfam International  amesema katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya Wanawake wa vijijini, ni wakati muafaka kwa serikali kutoa tamko kusaidia wanawake wa vijijini.." Programu za serikali lazima zielekeze hivyo kwani zina nafasi kubwa na ya msingi kuwatia hamasa wakulima wanawake na wahusika wa masoko" alisema mkurugenzi wa Oxfam International.

 

Hata hivyo aliendelea kusema Wanawake lazima wapewe kipaumbele katika program hizi za kilimo ili ziwasaidie kuongeza mavuno, kupambana na changamoto za miundombinu hususani usafiri na kutoa taarifa za masoko ya mazao kwa wakati stahiki. Ni dhahiri kwamba kwa kuwapa wanawake fursa za kufikia zana za uzalishaji kama ilivyo kwa wanaume ingepunguza idadi ya watu waishio na njaa ulimwenguni kwa kati ya watu milioni 100 - 150 "

 

Nchini Tanzania wanawake 6,744,000 wenye umri kati ya miaka 15-49 wanaishi maeneo ya vijijini. Na hii ni asilimia 66% ya wanawake wote wenye umri wa kati ya miaka 15-49 nchini Tanzania. Lakini basi, wanawake hawa wa vijijini ndio wenye nafasi ndogo ya kujifungua wakiwa na usaidizi wa mhudumu wa afya mwenye ujuzi kama vile daktari, afisa tabibu, muuguzi au mkunga.

Jumatano, 15 Oktoba 2014

SIKU YA MTOTO WAKIKE YAJA NA MJADALA WA NDOA ZA UTOTONI

Chama cha Wanahabari Wanawake nchini - TAMWA kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu duniani (UNFPA) na mashirika mengine yasiyo ya kiserikali wameungana katika kuadhimisha siku ya mtoto wakike Duniani yanayofanyika oktoba 10 kila mwaka kwa kufanya mjadala mpana juu ya kukomesha ndoa za utotoni hapa Tanzania.

Mjadala huo uliofanyika katika hoteli ya CMG-Motel mjini Tarime mkoani Mara na kufuatiwa na kilele chake kilichofanyika oktoba 11ni mwendelezo wa kampeni ya Kitaifa ya kutokomeza ndoa za utotoni ijulikanayo kama “Ndoa za umri mdogo, Ukanda Huru” iliyozinduliwa mwaka huu ikiwa na lengo la kuboresha mienendo ya Taifa kwa ajili ya kuhakikisha viongozi wanawajibika katika kukomesha ndoa hizo kwa kuweka mikakati ili wasichana wapate haki zao.

Mwaka 2011, Baraza Kuu la Umoja wa Mataia lilipitisha maadhimio ya kuanzisha Siku ya Mtoto wa Kike Duniani. Siku hiyo imetengwa kwa ajili ya kuendeleza,kukuza haki na kutatua matatizo yanayowakumba wasichana. Kauli mbiu mwaka huu ‘Kuwawezesha Wasichana: Kumaliza Mduara wa Ukatili’ ambayo inatoa wito kwa wadau mbalimbali kutambua umuhimu wa kuwekeza, kuwawezesha na kutokomeza aina zote za ukatili zinazowapata wasichana ikiwa ni pamoja na ndoa za utotoni.

Ndoa za utotoni ni suala linalohusu haki za binadamu; linakiuka haki za binadamu na kuzuia maendeleo kwa wasichana na wanawake. Aidha katika Tanzania pekee, wastani wasichana wawili kati ya watano wanaolewa kabla ya kufikia umri wa miaka 18 wakati katika bara la Afrika zaidi ya asilimia 42%  ya watoto wa kike wanaolewa kabla ya kufikia umri huo huku mamilioni wakiolewa wakiwa bado hawajafikia umri wa kubalehe. Vilevile nchi 31 kati ya 41 duniani ambapo mwenendo wa kuozesha watoto wa kike unakaribia asilimia 30% zimo Afrika.

Jumatatu, 13 Oktoba 2014

HOSPITALI YA AGHA KHANI YAFANYA UCHUNGUZI WA SARATANI YA MATITI KATIKA KUADHIMISHA SIKU YA UFAHAMU WA UGONJWA HUO

Hospital ya Aga Khan imefanya kambi ya bure ya uchunguzi wa salatani ya matiti  kwa kuadhimisha mwezi wa ufahamu wa saratani ya matiti duniani  huko jijini Dar es salaam

Mkurugenzi Mkuu wa hospitali hiyo, DK Mustafa Bapumia akizungumza na waandishi wa habari juu ya maadhimisho hayo.
 Kambi hiyo ya Afya imeshuhudia angalau watu 200 wakifanyiwa uchunguzi wa saratani ya matiti  pamoja na kupata ushauri nasaha kuhusu ugonjwa huo.
 
Akizungumza wakati wa tukio hilo Dk. Amyn Alidin mtaalamu wa saratani katika Hospitali hiyo, alieleza umuhimu wa kupima afya mara kwa mara jambo ambalo huhakikisha afya njema kwa wote.

Pichani ni akina mama wakichukuliwa waelezo kwaajiri ya afya yao
Kwa mujibu wa shirika la Afya Duniani kuna kesi mpya takribani 1,380,000 na vifo 45800 kutokana na saratani ya matiti kila mwaka. Wingi wa vifo hivyo 269,000 hutokea katika nchi zenye vipat vya chini ambapo wanawake wengi wenye saratani ya matiti huchunguzwa na kutambuliwa katika hatua za mwisho kutokana na ukosefu wa ufahamu wa kugundua mapema