Hayo yalisemwa jana na Kaimu Balozi wa japan nchini Kazuyoshi Matsu Naga wakati wa sherehe za mahafari ya pili ya shule hiyo yaliyofanyika jana na kuhudhuliwa na Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha Rose Migiro ambaye alikua mgeni rasmi baadhi ya viongozi wengine wakiwemo baadhi ya wake wa wageni wengine mbalimbali.
![]() |
| Waziri wa Katiba naSheria Dkt Asha Rose Migiro (katikati) Akiwa na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendereo WAMA Mama Salma Kikwete pamoja na Kaimu balozi wa Japani. |
Kwa upande wake, Dkt. Migiro, ambaye alikuwa mgeni rasmi
katika sherehe hizo, aliwataka wadau mbalimbali kuendelea kumsaidia
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Salma Kikwete
katika kusaidia wanafunzi hao ili kupanua fursa za watoto wa kike
kielimu
Naye Mke wa Rais Mama Kikwete, ambaye pia ni Mwenyekiti wa
Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) aliwataka wanafunzi hao
kutumia nafasi ya kusoma bidii ili waweze kufaulu hatimaye kushika
nafasi mbalimbali za uongozi kama Dkt.
Akizungumzia kuhusu matarajio ya WAMA kutokana shule hiyo, alisema kutoa wataalamu wa nyanja zote , ikiwemo fani ya sayansi . Hivyo aliwataka kuongeza bidii katika masomo ya sayansi. Alisema WAMA itaendelea kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu hadi watakapofikia hatua ya mwisho.
![]() |
| Wahitimu wa elimu ya sekondari kidato cha nne katika shure hiyo ya WAMA wakati wa sherehe yao ya kumaliza |
Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa Tamisemi (TAMISEMI) Hawa Ghasia aliwapongeza walimu
wa shule hiyo kwa bidii zao ambao zimeifanya shule hiyo kuongeza
katika wilaya hiyo.


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni