Wanawake nchini Tunisia wameendelea
kupigania haki zao ili kushika nyadhifa za kisiasa kwa mjibu wa katiba
ya nchi hiyo, hata hivyo baadhi ya wanawake wameanza kuonyesha wazi wazi
jitihada za kujikomboa kiuongozi.

Kama ambavyo walionekana baadhi ya wanawake wakiwa wamekaa mbele ya mti huku wakiandika baadhi ya dondoo mhimu katika mafunzo yanayotolewa na taasisi moja isiyo ya kiserikali kuhusiana na mafunzo ya kisiasa kwa wanawake hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa nchi hiyo.
" Wanawake nchini Tunisia wanatakiwa kujengwa katika kujiamini ili waweze kufikia hatua ya kushika vyeo vya kisiasa”anasema mwezeshaji mafunzo ya kisiasa kwa wanawake kutoka asasi isiyokuwa ya kiserikali ambayo imekuwa ikitoa mafunzo ya kuwapa ujasiri na mbinu za kisiasa wanawake ili waweze kugombea nyadhifa mbalimbali.
![]() |
| Wanawake wa Tunisia wakiwa kwenye warsha wakijifunza kujiamini na kujitathimini katika ulingo wa kisiasa. |
Katika kipindi ambacho wanawake wa nchi za kiarabu wanapigania haki zao, hali imekuwa tofauti nchini Tunisia ambako wanawake kwa uwazi kabisa wamefikia hatua ya kuelezea haki zao hadharani kushinikiza utekelezwaji wa katiba mpya iliyopitishwa mwaka huu inayosisitiza umhimu wa kuwa na wanawake katika vyeo vya kisiasa.
Sheria ya uchaguzi nchini Tunisia inaeleza kuwa katika majimbo yote ya uchaguzi 33 ni lazima kuwe na usawa kati ya wanawake na wanaume,hadi sasa kuelekea uchaguzi mkuu ujao ni aslimia 11.2 tu ya wanawake ndiyo waliopo katika orodha ya wanaowania uchaguzi huo.
Wanawake nchini Tunisia wana historia ndefu ya kudai ukombozi wao katika kushiriki kushika nyadhifa za kisiasa kama ambavyo maandamano ya Ennahda yaliyofanyika mwakajana.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni