Jumatano, 22 Oktoba 2014

WANAWAKE WAJANE WAANDAMANA KUDAI HAKI ZAO

Kikundi cha wanawake ambao ni wajane wameamua kuandamana hadi katika ofisi ya mkuu wa mkoa  wakimshinikiza kupata haki ya mali zao walizoachiwa na waume zao ambazo wamekua wakizifatilia kwa muda mrefu bila mafanikio  huko mkoani Morogoro.

Maandamano hayo ya amani yamefanywa na wanawake hao ili kumtaka Mkuu wa Mkoa atoe kauli yake kwa mamlaka usika ili kuakikisha wanapatiwa kwa haraka mali zao kutokana na kusubiria kwa muda mrefu bila mafanikio na kila wanapojaribu kufatilia upata usumbufu na kubadirishiwa tarehe za kufatilia.

"Tumeamua kuungana na kufanya maandamano haya ya amani ili kupaza sauti zetu kwa Muheshimiwa Mkuu wa Mkoa ili aweze kutusaidia kupata haki yetu tulioachiwa na waume zetu ikiwa walifanya kazi na hili tunalolitafuta sisi ni jasho waliloliangaikia kwa muda mrefu walipokua hai", alisema mmoja wa wanawake hao walioandamana.

Nae Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Bw.Joel Bendela amewahaidi wanawake hao wajane kwa kuwataka wawe na moyo wa uvumilivu huku yeye akivaa malalamiko yao kwa lengo la kuyatatua kwa haraka kama wanavyoitaji na kuwaambia kuwa ni haki yao na atafanya uchunguzi kwa yeyote mwenye lengo la kuwazurumu haki yao itakapo bainika atawaajibisha

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni