Jumanne, 28 Oktoba 2014

MWANAMKE APIGWA NA MUMEWE HADI KUFA HUKO MKOANI MOROGORO

Bado ukatiri unaofanywa na wanaume kwa wake zao unaenderea kuripotiwa huku ikiwa jamii ikitahayari kuona Katibu mkuu wa CCM Mkoa wa morogoro Bi. Rozina kopa ameuwawa baada ya kupigwa na mumewe huku chanzo cha kupigwa kwake adi kufa bado hakijafahamika.

Marehemu bi. Rozina kabla ya kifo chake inasemekana baada ya kukorofishana na mumewe nyumbani aliamua kuondoka ili akwepe ugomvi kuenderea ndipo mtuhumiwa wa mauaji hayo Hamis Tata ambaye ni mume wa marehemu alimsaka tena mkewe na ndipo alipomkuta kwenye bar ya mafiga bar na kuanza kumpiga.

Mashuhuda wa tukio hilo akiwemo bwana mmoja aliyefahamika kwa jina la Rajabu alisema yeye ameshuhudia tukio hilo na alijaribu kumzuia mtuhumiwa kumpiga huku marehemu akionekana anavuja sana damu hasa sehemu za usoni na ndipo mtuhumiwa alimuacha kumpiga mkewe.

 Kwa upande wa  ndugu wa marehemu wamesema ndugu yao baada ya kupigwa sana pale bar waliporudi nyumbani mtuhumiwa aliendelea kumpiga mkewe na kumuingilia kimapenzi bila idhini yake
kabla mauti haijamkuta walimkimbiza hospitali ya mkoa uku akiwa akilalamika kifua kumuuma sana .

Naye kamanda wa polisi mkoani morogoro amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na adi sasa wanamshikiria bw. Hamis Tata kwa tuhuma za mauaji.

Hili ni moja ya tukio baya ambalo bado linazidi kuongeza idadi ya vifo vya kinyama vinavyofanywa na wanaume kwa wake zao na hatimaye mwili wa Bi Rozina Tata umezikwa katika makaburi ya kora huko mkoani Morogoro.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni