Mwanadada Lorraine aliyeiwakilisha Tanzania katika mashindano ya urembo ya kimataifa ya Miss Grand International 2014, na kufanikiwa kushika nafasi ya 20 bora katika shindano lilofanyika mjini Bangkok Thailand ametua nchini jana Oktoba 9 majira ya saa 10 jioni na kuwashukuru watanzania kwa kumuunga mkono.
| Mrembo Lorraine clementi pichani akipungia watu walieenda kumpokea uwanja wa ndege wa Kimataifa jana. |
Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es salaam, Lorraine aliwashukuru wadau mbalimbali kwa kufanikisha ushiriki wake kwenye mashindano hayo makubwa duniani.
"Pondezi kwa wadau wote mliofanikisha mimi kupeperusha vyema bendera ya Tanzania". alisema Lorraine.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni