Jumatatu, 6 Oktoba 2014

UMOJA WA WABUNGE WANAWAKE BUNGENI WAIPONGEZA RASIMU YA MWISHO YA KATIBA

Umoja wa Wabunge Wanawake Tanzania (TWPG)  wamejipongeza kwa hatua kubwa waliyofikia na manufaa waliyoyapata wanawake katika Rasimu ya mwisho ya katiba inayopendekezwa.
 
 Kauli hiyo imetolewa Bungeni Mjini Dodoma na Wabunge hao ambao pia ni Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakati walipofanya semina iliyoandaliwa kwa ajili ya wajumbe hao kuhusu maandiko ya kisheria na manufaa waliyopata wanawake katika Rasimu ya mwisho ya Katiba inayopendekezwa.
 

Mh Angella Kairuki  Ktibu Mkuu wa TWPG wakati akiwasilisha hoja katika semina iliyofanyika Dodoma
 Akitoa mada wakati wa semina hiyo, Katibu Mkuu wa TWPG ambaye pia ni Mjumbe wa Bunge hilo Mhe. Angellah Kairuki amesema kuwa moja ya manufaa ambayo wanawake watakayopata katika Katiba mpya ijayo ni kuhusu masuala ya uongozi ulio bora wenye kuzingatia sifa na weledi katika michakato ya ajira  na utetezi ambao suala hilo limetiliwa nguvu katika ibara ya 208, Ibara ndogo ya kwanza kipengele C ambacho katika maswala ya utetezi na mambo ya ajira katika nafasi mbalimbali katika Utumishi wa Umma utazingatia uwezo wa kitaaluma, weledi, ujuzi, usawa wa jinsia hivyo suala la usawa wa jinsia umezingatiwa.
 
Mhe.Kairuki ameongeza kuwa, katika sura ya kumi inayohusu masuala ya Bunge kama ilivyoelezwa katika Ibara ya 129 ibara ndogo ya nne, amesema kuwa kwa kutambua kuwa Bunge kama muhimili muhimu wa dola Katiba inayopendekezwa imekusudia kurekebisha kasoro iliyopo ya uwakilishi mdogo wa wanawake Bungeni ambapo hivi sasa kuna asilimia 36.6% ya wanawake.
 
"Kupitia Rasimu hii inayopendekezwa kupitia ibara ya 129 Ibara ndogo ya nne tutakua na uwakilishi uliosawa baina ya wabunge wa wanawake na wabunge wanaume", alisema Mhe. Kairuki.
 
 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni