Bado jamii aijaelewa na kutambua kuwa mwanamke nae ana haki ya kumiliki ardhi na kusababisha mgogoro mkubwa kuendelea huku baadhi ya wanawake wameanza kuelewa haki zao na kuanza kupigania.
Serikali imeweka dhamira ya dhati katika kuhakikisha mwanamke anatakiwa kupata haki sawa na mwanaume pia na kuweka mkakati wa kuweka sheria ambayo inamruhusu mwanamke kumiliki ardhi.
Hata hivyo chama cha wanasheria wanaweke nchini Tanzania (TAWLA) kimeamua kufanya utafiti kuhusu migogoro ya ardhi inayowakabiri wanawake na kurudi na majibu ambayo utafiti huo uliosisha mikoa ya Dar es salaam na Tanga.
Mwenyekiti
wa Chama cha Wanawake wanasheria Tanzania (TAWLA) Aisha Bade (kulia)
akitoa ufafanuzi
Vile vile Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake wanasheria Tanzania Aisha Bade amesema lengo la kufanya tafiti hiyo ni kufahamu wanmeathirika kiasi gani ili kuhakisha kuwa wanawake nao wanaweza kumiliki ardhi kwa mujibu wa sheria ambayo itapitishwa.
Pia wamewataka wanawake kuwa na misimamo yao ambayo itawasaidia kutopoteza haki zao za msingi na kutoficha matatizo ambayo wanakumbana nao na kuweka adharani ili kufanya kupata misaada ya kisheria.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni