Alhamisi, 16 Oktoba 2014

SIKU YA KIMATAIFA YA WANAWAKE VIJIJINI YAFANYIKA JANA KWA LENGO LA KUWASAIDIA HASA KWENYE SEKTA YA KILIMO

Ikiwa jana ni siku ya kimataifa ya wanawake wa vijijini, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amesema kundi hilo linaweza kuchagiza maendeleo ya dunia iwapo sauti na mahitaji yao yatazingatiwa. Maadhimisho hayo yamefanyika jana oktoba 15 yakiwa na lengo la  Kuwaunga mkono wakulima wanawake kwa lengo kuwasaidia kushinda balaa la njaa.

 

 

Na kwa hapa nchini Tanzania  Mkurugenzi wa Oxfam International  amesema katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya Wanawake wa vijijini, ni wakati muafaka kwa serikali kutoa tamko kusaidia wanawake wa vijijini.." Programu za serikali lazima zielekeze hivyo kwani zina nafasi kubwa na ya msingi kuwatia hamasa wakulima wanawake na wahusika wa masoko" alisema mkurugenzi wa Oxfam International.

 

Hata hivyo aliendelea kusema Wanawake lazima wapewe kipaumbele katika program hizi za kilimo ili ziwasaidie kuongeza mavuno, kupambana na changamoto za miundombinu hususani usafiri na kutoa taarifa za masoko ya mazao kwa wakati stahiki. Ni dhahiri kwamba kwa kuwapa wanawake fursa za kufikia zana za uzalishaji kama ilivyo kwa wanaume ingepunguza idadi ya watu waishio na njaa ulimwenguni kwa kati ya watu milioni 100 - 150 "

 

Nchini Tanzania wanawake 6,744,000 wenye umri kati ya miaka 15-49 wanaishi maeneo ya vijijini. Na hii ni asilimia 66% ya wanawake wote wenye umri wa kati ya miaka 15-49 nchini Tanzania. Lakini basi, wanawake hawa wa vijijini ndio wenye nafasi ndogo ya kujifungua wakiwa na usaidizi wa mhudumu wa afya mwenye ujuzi kama vile daktari, afisa tabibu, muuguzi au mkunga.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni