Waziri wa Afya na ustawi wa jamii Dkt. Seif Rashid amesema matumizi ya dawa hayo yapo salama kwa mtumiaji na hivyo kuwataka wazazi wakubaliane katika kufanya maamuzi ya kutumia dawa hizo ili kujenga familia iliyo bora isiyokua na ugumu wa kuendelea hii itasaidia kupunguza idadi ya watoto wa mitaani Alisema hayo wakati akikagua utekelezaji wa mipango yake katika mkoa wa Shinyanga.
Aliendelea kusema kuwa wanawake wanatakiwa kufika katika vituo vya afya vilivyo karibu nao ili kupatiwa vipimo na ushauri kabla ya kutumia dawa izo ili kuakikisha afya zao zinakua nzuri na pindi wanapokua tayari kwa kupata mtoto mwingine waweze kwa wakati.
Hata hivyo watoto wa mitaani wamekuwa wengi ambao wameonekana wakiomba omba mitaani huku wengi wao wakikosa haki zao za msingi kama elimu huku wengine wakijiunga katika makundi hatarishi kama ulevi japo zipo sababu mbalimbali zinazosababisha lakini tatizo la wazazi kutokua na uzazi wa mpango unawafanya kushindwa kumudu kutekeleza mzjukumu kwa watoto wao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni