Hata hivyo, wataalamu wa afya wanaonya na kusema kuwa nguo hizi za mitumba, hususan za ndani zina madhara mengi kwa wanawake na wanaume wanaopenda kuzitumia.
Hivi karibuni, Shirika la Viwango Tanzania (TBS), limepiga marufuku na kutoa kipindi cha mwisho kwa wafanyabiashara hao wanaouza nguo za ndani za mitumba, kuacha kuuza bidhaa hizo.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya kipindi cha mpito kuisha, ambapo kwa sasa TBS wamechukua uamuzi wa kuzichoma moto nguo hizo.
Msemaji wa TBS, Rhoida Andusamile anasema hatua hiyo ni utekelezaji wa matakwa ya agizo la sheria ya mwaka 2009 inayozuia matumizi ya nguo za ndani zilizokwishatumika.
Msemaji wa TBS, Rhoida Andusamile anasema hatua hiyo ni utekelezaji wa matakwa ya agizo la sheria ya mwaka 2009 inayozuia matumizi ya nguo za ndani zilizokwishatumika.
Profesa Malise Kaisi wa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba Shirikishi Muhimbili (Muhas) anasema, yapo madhara makubwa ya kuvaa nguo za ndani za mitumba kutokana na unyeti wa maeneo yanapovaliwa nguo hizo.
Anasema, walioketi juu ya hatari zaidi ni wanawake ambao maumbile yao yapo wazi zaidi na ni rahisi kwa vijidudu kuingia kwa urahisi pindi wanapokaribia vitu hatarishi. Kwa mfano, anasema, nguo za ndani zilizovaliwa huenda zina vijidudu vya fangasi au chawa wa sehemu za siri, mwanamke anapovaa hupata maambukizi hayo.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni