Jumanne, 7 Oktoba 2014

MWANAMKE AKIOLEWA KUNA ULAZIMA AITWE JINA LA UKOO WA MUMEWE?

Tangu miaka na miaka wanawake walio wengi wakiolewa upenda kubadirisha majina ya wazazi wao au ya ukoo wao na kutumia ya waume zao hasa ya ukoo.

Wapo viongozi wengi na watu wengi ambao wameacha majina yao na kutumia ya waume zao wapo wake wa Maraisi ,Mawaziri wakuu mfano Mama Salma kikwete, Mama Tunu Pinda na wengine wengi na kufanya kuzidi kuheshimika na wao pia hutumia vizuri majina hayo.

Kutumia jina la mumeo ni uamuzi wa mwanamke mwenyewe lakini hakuna sheria inayomwongoza mwanamke pindi aolewapo atumie jina la mumewe.





Kwa miaka ya karibuni baadhi ya wanawake wengi wameachana na dhana au utaratibu huo, na kutoa hoja ya kwamba hawaoni sababu ya kutumia majina ya ukoo wa waume zao baada ya kuolewa.

Wengi ya wanawake niliobaatika kuzungumza nao walionekana kupinga matumizi ya majina ya waume zao kwa hoja kuwa kwa ndoa za siku hizi ni kujisumbua tofauti na zamani zile za mababu na mabibi zetu kutokana na wao kudumu na ndoa zao.





 "Ila kwa sasa ukitumia jina la mumeo na likazoeleka kesho ukiachana nae kurudi kwenye jina lako unakua mgeni kwenye jamii hali hii inasababisha wanawake wengi tukiolewa  tunapenda kuendelea nakuitwa kwa majina ya ukoo wa wazazi wetu" alisema mama Patric, mkazi wa Mabibo Jijini Dar es salaam.

Ndoa kama inavyotakiwa kuwa na uvumilivu ili idumu ndiyo silaha ya matumizi ya majina ya waume lakini wapo wanawake walioachwa kwa talaka au kufiwa, waliendelea kujulikana kwa majina ya waume zao bila kuathiri maisha. Mfano, Winnie Madikizela Mandela na Graca Simbine Machel.






Swali la msingi kuliko yote, kwamba kuna ukweli wowote ndoa za siku hizi hazitoi fursa kwa mke kutumia jina la mumewe?

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni