Hospital ya Aga Khan imefanya kambi ya bure ya uchunguzi wa salatani ya matiti kwa kuadhimisha mwezi wa ufahamu wa saratani ya matiti duniani huko jijini Dar es salaam.
Kambi hiyo ya Afya imeshuhudia angalau watu 200 wakifanyiwa uchunguzi wa saratani ya matiti pamoja na kupata ushauri nasaha kuhusu ugonjwa huo.
Akizungumza wakati wa tukio hilo Dk. Amyn Alidin mtaalamu wa saratani katika Hospitali hiyo, alieleza umuhimu wa kupima afya mara kwa mara jambo ambalo huhakikisha afya njema kwa wote.
Kwa mujibu wa shirika la Afya Duniani kuna kesi mpya takribani 1,380,000 na vifo 45800 kutokana na saratani ya matiti kila mwaka. Wingi wa vifo hivyo 269,000 hutokea katika nchi zenye vipat vya chini ambapo wanawake wengi wenye saratani ya matiti huchunguzwa na kutambuliwa katika hatua za mwisho kutokana na ukosefu wa ufahamu wa kugundua mapema
| Mkurugenzi Mkuu wa hospitali hiyo, DK Mustafa Bapumia akizungumza na waandishi wa habari juu ya maadhimisho hayo. |
Akizungumza wakati wa tukio hilo Dk. Amyn Alidin mtaalamu wa saratani katika Hospitali hiyo, alieleza umuhimu wa kupima afya mara kwa mara jambo ambalo huhakikisha afya njema kwa wote.
| Pichani ni akina mama wakichukuliwa waelezo kwaajiri ya afya yao |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni